Thursday, March 25, 2010

Utajitambuje Kama Unaakili???????????????????????


KWA mujibu wa Mwanasaikolojia mwenzangu Howard Gardiner aliandika kuwa binadamu wanatofautiana kiakili kila binadamu anauwezo wake katika kufikiri.

Sasa ndugu mpenzi wa blogu hii, utajitambuaje kuwa wewe unaakili kiasi gani? Wewe na wenzako munatofautiaje katika kufikiri? Kulingana na akili uliyonayo unatakiwa uwe nani na uishije katika dunia hii?

Jibu la maswali hapo juu ni kwamba ili kujitambua akili yako unatakiwa kuwafanya mahesabu ya akili yako. Na kwa mujibu wa Gardiner unatakiwa kufuata fomula hii hapa chini:

Chukua Akili ya Umri wako gawanya kwa Mtiririko wa Umri wako na Zidisha kwa Miamoja = Akili yako.

Akili= Mental Age (MA)            x    100
          Chronological Age (CA)

Kama mental age ni kubwa kuliko chronogical age jua kuwa akili yako iko juu zaidi ya kawaida, kama mental age iko sawa na chronological age jua kuwa akili yako ipo katika hali ya kawada na kama mental age iko chini ya chronological age jua kuwa akili yako iko chini ya kawaida.

Sasa jitambue wewe uko katika hali gani jifanyie uchunguzi ili kujitambua zaidi fanya mahesabu ya kujua akili yako ili uweze kujikonturo na maisha, jiwekee malengo kwa kufuatana na uwezo wako wa kufikiri. Ni hayo tu mpenzi wa blogu hii na kama unapenda zaidi kujifunza juu ya habari hii bonyeza katika kifungu cha kuchangia maoni na acha maelezo yako hakika nitayafanyia kazi.Zaidi kujitambua ni muhimu katika maisha yako

Sunday, March 21, 2010

Penzi ni Tamu Sana Jaribu Uone???



PENZI ni tamu sana kila mtu anatambua hilo, na kukoswa pendo ni uchungu sana katika maisha ya binadamu.

Pamoja na hayo yawezekana wewe unayesoma blogu hii na wewe unampango wa kumuacha mpenzi wako, kutokana na sababu mbalimbali lakini yote hayo ni sawa na kupotea ndugu yangu.

Nakuomba sana usimuache mke wako kwani daima ulishamutamkia kuwa unampenda na hutamuacha kamwe katika maisha yako! Kumbuka baada ya kumuacha mrembo bibie utapata nini au utafaidika na nini? Zaidi ya kuanza kujuta na kuumia roho yako?

Wapo wanaume wengi wanaoachana na wake zao matokeo yake wanaanza kujutia kitendo hicho.

Namkumbuka baba mmoja tajiri mkubwa katika jiji hili la Dar aliwahi kuja katika ofisi zetu za ushari ili kuomba ushari wa doa yake
Baada ya mke wake kuchoshwa na baba huyo na kuamua kurudi kwao Mwanza.

Sasa baada ya kuachwa baba huyo alianza kuumia zaidi na kuwa anashinda nyumbani badala ya kwenda kazini, jambo ambalo lilimpelekea kuja ofini kwetu kuomba ushauri wa kufanya ili mke wake arudi.
Nasi tulimpatia ushauri na tukamuita mke wake naye tukamupa ushauri wa umuhimu wa mke na mume katika ndoa, jambo ambalo liliwaunganisha na mpaka sasa wanaishi kwa amani na upendo wa ajabu.

Sasa ndugu yangu kumbuka kuwa mwanamke ni muhimu sana katika maisha yako, mwanaume ameumbwa kwa ajili ya mwanamke na mwanamke kwa ajili ya mwanaume sasa kunahaja gani ya kumtukana mke wako ambaye ni mzuri? Kunahaja gani ya kumfukuza mke wako anaye kupa penzi la dhati? Na kunahaja gani ya kuwa na msongo wa wawazo kisa mke wako mwenye penzi tamu kaondoka? Sasa mwambie mke wako nakupenda sana mke wangu na sitakuacha kamweeeee.

Jitambue

BINADAMU tumezaliwa kuwaza kila wakati Mwanasaikolojia Alfred Binett mtaalamu wa mambo ya Intelligent Quotients (IQ) alisema kuwa ndani ya dakika moja binadamu huwa anawaza mambo mengi sana.

Kwa hiyo ili kufikia malengo na mikakati ya maisha yako unatakiwa kujitambua uko katika sehemu ipi hasa unapowaza mikakati ya maisha yako.

Usikubali kuyapa nafasi kubwa mawazo yasiyokuwa na manufaa katika maisha yako jitahidi kuyatupilia mbali na kukubaliana na mawazo ambayo yatakuletea manufaa, amini kuwa hujazaliwa masikini bali umezaliwa kuishi kutokana na unavyotaka.

Kumbuka kuwa mikakati ya mawazo yako ndiyo yatakufanya ufikie malengo, anza sasa kuwaza mafanikio hakika utaona.

DIGITAL MEDIA PRODUCTIONS LTD

Watengenezaji wa vitambulisho, business cards, matangazo mbalimbali ikiwa pamoja na kupiga photocopy, kuprint vipeperushi, vitabu, magazeti, majarida ya kila aina sasa wamekupunguzia bei.

Kwanini uhangaike? wakati DMPL wapo kwa ajili yako, lete kazi yako sasa tutaitengeneza kwa kiwango cha hali ya juu.

Kwa maelezo zaidi fika chuo kikuu cha Dodoma block “F” chumba nambari 74 au wasiliana nasi kwa simu: 0764 992264, 0719 020253 au tuandikie: 1982leonard@live.com




LAPTOP INAUZWA

Laptop yenye rangi ya silver, speed processor 1.735, Pentium M, screen kubwa inahali nzuri inauzwa kwa bei poa. Kama unahitaji kwa shughuli zako mbalimbali wasiliana kwa simu 0719 020253, 0764 992264.

Tangazo be the partnerof profits

BLOGU yako ya Saikolojia bado inakaribisha matangazo kwa wale wote wanaotaka kutangaza biashara zao kupitia mtandao huu unaangaliwa dunia nzima.

Kumbuka kuwa biashara ni matangazo, tangaza biashara yako upate faida zaidi na zaidi hakika mtandao wa Saikolojia unalipa zaidi.

Kwa maelezo zaidi wasiliana nasi kwa simu: 0764 992264 au 0719 020253 kwa e-mail: fitazi@hotmail.com



PSYCHOLOGY blog now welcome you to advertise your business on this blog which is viewed by all people around the world.

Remember that business is a partner of ADVERTS, make more profits through advertisings & remember that Psychology blog pays.

For more information contact us: +255 764 992264, +255 719 020253, e-mail: fitazi@hotmail.com