Haya ndugu zangu napenda kuwaarifu kitu ambacho ninataka kukifanya kwa sasa hivi. Kitu hicho ni kwamba nataka kwenda kusoma chuo kwani wahenga walituambia ya kwamba "Elimu Haina Mwisho" na kitabu kitakatifu kinatuambia ya kuwa "Mshikeni Elimu Msimuache aende zake maana huyo ni uzima wetu" kwahiyo wanablogu wenzangu nataka niendelee kufuata haya maandiko ili nione kama yanaukweli.
Ila ninatumai tuko pamoja popote nitakapokuwa, Bwaya, Markus mpangala, Dada Yasinta, Da Koero, na wengine Mungu awabariki sana.