Monday, December 15, 2008

Nguvu ya penzi tumepewa na Mungu


Huwa ninajiuliza hivi penzi ni kitu gani? penzi lilitoka wapi? kwanini ukipenda kuzidi kiasi unakuwa kama kipofu? kwanini penzi linawafanya watu kubadilika? Kwanini penzi linaua yaani mtu anaamua kujiua kisa kakataliwa na mpenzi wake? Au anaamua kumuua mtu aliyemchukulia mpenzi wake?


Yote haya ni nguvu ya penzi ambalo tulipewa na Mungu kwakweli penzi ni kitu kitamu sana tena sana!! hakuna kitu cha muhimu katika dunia hii kama penzi.


Binadamu hata kama munapendana kiasi gani ukimchukulia mpenzi wake urafiki unaisha na munakosana kabisa ikiwezekana hata kufanyiana mambo mabaya. Hata baadhi ya wanyama ukiwakuta wanafanya mapenzi huwa wakali wanaweza kukurarua ukiwasogelea wakizani utawanyang'anya wapenzi wao.


Jamani penzi ni kitu gani? Kwanini penzi linakuwa hivyo?

Mwanaume anachelewa kurudi nyumbani


"Najitahidi sana kumshauru mme wangu Leonard ili awe anawahi kurudi ili nimufaidi mme wangu lakini hataki kutekeleza ushauri wangu sasa ngoja kuna siku nitaenda kumchongea kwa bosi wake ili afukuzwe kazi nifaidi penzi lake kwa kuwa naye masaa yote" alisema dada mmoja ambaye anafahamika kwa jina la Mariam Sabaganga mkazi wa Mwanza.


Pengine wa wewe unamawazo kama hayo kutokana na mme wako kutingwa na kazi nyingi na hatimaye kushindwa kuwa anawahi kurudi nyumbani mapema. Nakuomba usiwe na wivu kiasi hicho kwani kazi ya mme wako ndiyo inawafanya kuishi au kujiongezea kipato nyumbani kwenu.


"Ninajuta sana kutokana na watoto wetu kushindwa kusoma kutokana na mme wangu kufukuzwa kazi baada ya kumchongea kwa bosi wake kuwa anatabia ya kumuibia bosi pesa za kampuni yake na kuleta nyumbani na zingine kuweka benki" alisema mama Aisha mkazi wa Area "D" mjini Dodoma baada ya kujuta kutokana na kumsababishia mme wake kufukuzwa kazi kwa wivu wa mapenzi.


Aliendelea kusema kuwa "Kama ningejua kama tutateseka kiasi hiki, yaani tunalala njaa huku watoto hawaendi shule, kwakweli inaniuma sana na ninamuomba Mungu atusaidie angalau tupate pesa za kuwasomesha Aisha, Ben na Hamis!"alisikitika mama huyo.


Sasa je, na wewe unawivu wa kiasi hicho? Toa maoni yako ili kusaidia kufanikisha kwa utafiti ambao unafanya na shirika la Tanzania Women Reseach.

Kazi ya uandishi wa habari

NINAPOSEMA Mwandishi wa habari kwa maana nyingine ninamaanisha Mtangazaji, Sasa ndugu zangu wasomaji wa blogu yenu ya saikolojia tunaambiwa ya kwamba mtu ambaye anafanya kazi ya kutangaza anatakiwa kuwa makini sana katika kazi hiyo, akiendana na kuwa mbunifu wa jambo kila siku.

Sasa basi kuhusiana na jambo la mapenzi Mtanzaji wakati ukiwa ndani ya studio unatangaza kipindi chochote unatakiwa kuondoa fikra za migongano au mikasa ya mapenzi iliyokupata aidha kutoka kwa mpenzi wake au sehemu nyingine.

Mtaalam wa Masuala ya mapenzi ambapo pia ni Mtangazaji wa Classic Fm Evas Chris aliwahi kufanya utafiti na kukundua kuwa asilimia 96 ya watangazaji wanaopata misukosuko kutoka kwa wapenzi wao mara nyingi wanafanya vibaya katika vipindi kutokana na kufikiria misukosuko ya wapenzi wao.

Chris katika tafiti yake hiyo ambayo aliita kwa jina "Good Presenter Research" alibaini kuwa wanandoa wengi ambao walikuwa katika hali ya kukosana na wapenzi wao walifanya vibaya katika media.


"Nilimshauri Denis Jakky kila mara aachane na mke wake kutokana na mke huyo kumfanya amfikirie yeye hata wakati ikiwa anatangaza kitendo ambacho kilimfanya kushindwa kutangaza vizuri" alisema Jeff Jeakim Mtangazaji wa Mercy Fm iliyoko Texas USA.

Tabasamu ni nguvu ya penzi

IMEELEZWA kwamba mtu ambaye anatabasamu kila wakati huwa anaonekana mzuri na mtanashati kuzidi mtu ambaye saa zote yeye ni kununa tu. Wataalam mbalimbali wa masuala ya saikolojia wamefanya tafiti juu ya jambo hili na kubaini vitu kama hivyo.Wataalam kutoka Chuo Kikii cha Haverd nchini USA, walifanya utafiti na kubaini mtu ambaye ananuna kila wakati huwa anazeeka mapema na huonekana mbaya wa sura kutoka na sura yake kuzoea kujikunja.

Ikiwa naye Mtaalam wa Saikolojia ya Mapenzi Richard Athony wa Uingereza katika utafiti wake anasema "Wanawake wanaochukia ndoa zao wengi wanaoneka kama wazee kutokana na kutokuwa na raha Wanawake wanatakiwa kuzifurahia ndoa zao ili kuepuka kuzeeka mapema" alisema Mtafiti huyo na kuongeza kuwa: "Uzee huo unatokana na kukoswa raha kila wakati jambo ambalo linawasababisha kutokujijari ikiwemo kuoga vizuri na kujipodoa" Je wewe mfuatiliaji wa blogu yako ya saikolojia umefanya utafiti juu ya suala hili na umegundua kitu gani? Changia maoni yako.