SIKU moja nilikuwa naelekea kwenye press conference moja tukiwa na rafiki yangu ambaye ni mwanahabari mwenzangu tulipofika maeneo ya Magomeni akaniambia kuwa anataka kuoa nami nikatafakari kwa kina maelezo kisha nikamjibu kuwa ni jambo jema kuoa kwani kuwa na mke ni mojawapo ya maisha tuliopangiwa na Mungu.
Mara nikakumbuka usemi wa Mwanafalsafa wa Kigiriki aitwaye Socrates naye alidhamini sana ndoa kwani aliwahi kusisitiza kuwa kama ukiona maisha ni magumu ni vizuri kuoa mwanamke Mzuri. "If you see life is hard you have to find a good wife to refresh your mind" alisema Socrates.
Jambo la kuwa na Mwanamke ni mhimu sana kwani watu wengi hasa katika nchi zinazoendelea huwa wanapata msongo wa mawazo kutokana na maisha kuwa magumu lakini Mwanasayansi Samuel Spire anasema kuwa kuwa na Mwanamke ni mojwapo ya kupunguza msongo huo wa mawazo.
Anasema kuwa mwanamke anasaidia kuondoa msogo wa mawazo kwa mwanaume vilevile mwanaume anasaidia kuondoa msongo wa mawazo kwa mwanamke. Hii inatokana na homoni zinazotolewa pindi mwanaume au mwanake anapokuwa na mpenzi wake.
Je , wewe ndungu yangu ulishawahi kukutana na msongo wa mawazo baadaye ulipomuona mpenzi wako ukajisikia uko fresh? sasa tujadili katika kibaradha chetu.