Sunday, May 17, 2009

Falsafa na Penzi


NIMERUDI tena ndugu zangu nilikuwa masomoni kwa muda kidogo ila sasa hivi niko kazini kwangu ninachati na mhariri wangu wa habari ambaye ndiye Mwalimu wangu Mkuu katika kuhakikisha jamii inaelimika kupitia vyombo mbalimbali vya habari.
Huko masomoni nimejifunza mambo mengi sana nimejifunza kuwa kumbe watanzania waliowengi hawajui kingereza!!!! Nilishaangaa sana Mhadhiri wangu wa lugha aliponiambia hata Kenya hawajui kingereza!!
Kwa sababu fani yangu ni Kudadisi nilimhoji kwa nini anasema hivyo ? Jibu alilonipa Ahhh!!! eti katika vitabu alivyosoma hakuna sehemu ambayo amekuta kumeandikwa rafudhi ya kingereza ya Afrika Mashariki!!(East African Accent) hayo yote nimejifunza kwa sababu nilikuwa nafuatilia kwa ukaribu sana mongozi wa lugha hii ya kingereza.
Ama kweli elmu haina Mwisho kwani nilijifunza mengi sana? Ikiwa pamoja na Mhadhiri wangu wa Falsafa alinifundisha kuwa elimu haina Mwisho huku akisema elimu inaanzia mtu anapozaliwa na pale anapokufa!!. Kwasababu napenda Falsafa niliamua kuziunganisha falsafa za Mhadhiri wangu na kuzifanyia kazi.
Jambo nililogundua ni kwamba hata penzi halina mwisho pendo linadumu siku zote ila kunakumchukia mtu fulani, lakini pia ukimchukia huyu utampenda huyu ndiyo maisha ya binadamu. Je kama tusingekuwa na upendo tungeishije katika dunia hii? Sasa tujadiliane ndugu zangu.