Wednesday, November 5, 2008

Furaha ya Harusi


Binadamu ameumbwa na elementi chocgezi za kureta furaha, huzuni, hasira, kucheka, kuchukia n.k, lakini binadamu tuliowengi tukiwa tunafunga ndoa huwa tunajawa na fura kubwa sana, lakini baada ya kuanza kuishi na mke au mme furaha inapotea kunazuka kuchukiana na ugonviwakati mwingine.


Hii ni hatari kweli ndugu mpenzi msomaji wa blogu yako hii! ila kwa ushauri wangu nakuomba hata kama umeikia katika maisha ya kuishi na wako kipenzi nakuomba usimuchoke kwani kumuchoka ndiyo chanzocha ugonvi, kununiana, hasira nk.


Machozi ya Penzi


Watu wengi hutoa machozi pale wanapoachwa na wapenzi wao, Mpenzi msomaji wa blogu yako uipendayo ya saikolojia leo nitakueleza kuhusiana na chozi la penzi: Unajua wataalamu wa mambo ya mapenzi wanasema kuwa Mwanamke ni mwepesi sana kutoa machozi pindi anapoachwa na mpenzi wake hii inatokana na mwanamke kuubwa na moyo wa kuwa na penzi la rohoni.


Wataalamu wa mambo ya mahaba wanasema kuwa wanawake wameumbwa kwa penzi la rohoni yaani la ndani tofauti na wanaume, hii ndiyo inasababisha mwanake akiachwa na mpenzi wake hujisikia vibaya na kujiona kama hafai kabisa kwa mwanaume yoyote kitendo ambacho kinamfnya anatoa machozi kwa wingi.


Mwanaume kaumbwa kwa penzi la fikra kama wanavyotufahamisha wataalamu wa mapenzi hii ndiyo maana wanaume wengi ni vigumu sana kulia pale wanapoachwa na wapenzi wao japo wapo wanaolia lakini sio wengi japokuwa huwa wanaumia sana rohoni lakini kutokana na elementi walizoumbwa nazo inakuwa vigumu kutoa machozi. "Nakusihi uendelee kuburudika zaidi na blogu yakousisahau kutoa maoni"