Sunday, December 28, 2008

Utamu wa mapenzi unafanana na nini?

BILA shaka msomaji wa blogu hii unampenda sana wako kipenzi na yawezekana unafanya kama huyo hapo kwenye picha anavyofanya kuonyesha kuwa mnapendana sana, na ikifika wakati wa chakula cha usiku unabonyeza/ unabonyezwa vizuri tu na unasugua kwa uraini huku utamu wa mpenzi wako unausikia vizuri.

Ebu fikiria iwapo inatokea siku moja, mpenzi wako akakusaliti na kwenda kumpa chakula cha usiku mtu mweingine utajisikiaje? au itokee siku mpenzi wako akaamua kukuacha na kwenda kuolewa na mtu mwingine.

Fikria maumivu utayoyapata ni ya aina gani? Hakika penzi ni tamu kwelikweli hasa kwa yule anayempenda kwa moyo wote. Sasa tujadiliane unasemaje?

Penzi linahitaji uvumilivu


WAKATI mwingine huwa unajisikia kumchoka mpenzi wako, kuchukua jukumu la kumuacha wako mpenzi, kumkaripia wako mpenzi, kumuona kama anakasoro fulani hivi, kumuona hakufai au hafai kuishi na wewe ikiwa pamoja na kutamani kuoa au kutafuta mwingine mpenzi.


Yote haya mambo huwa yanatokea kwa binadamu wa jinsia zote. Sasa nakuuliza kwanini unafikia hatua ya kufanya mambo kama hayo? Kama kweli uliamua kumpenda mpenzi wako ya nini tena kumchukia na kumuona hakufai?


Watalaam wa masuala ya mapenzi wanabainisha kuwa kumchukia mpenzi kunasababishwa na vitu vingi sana, ambapo mwanasaikolojia na mtaalam wa masuala ya love Haliet Julliu alifafanua katika kitabu chake cha "Bad Love - 2008" kuwa jambo la kwanza ambalo linamfanya mpenzi wako kukuchukia ni:


i)Uchufu wa mwili wako pia unapokuwa mchafu ndio unaongeza hatari ya kuchukiwa na mpenzi wako.


ii)Uchafu wa nyumba au chumba ambacho unakaa na mpenzi wako hasa hili linawahusu mwanawake, jambo hili huwa linawakera wanaume.


iii) Kupata mpenzi nje ya ndoa pia kunachakia mpenzi wako kukuchoka na kukuona hufai kisa kapata wa kumhodomola hasa akimpata anayejua mapenzi.


iv) Wewe mwenyewe kuwa mkali pindi unapomuona mpenzi wako nako kunachangia kumfanya atafute mwingine ambaye ni mpole ili apate kuliwazika zaidi kimahaba na,


v) Kuwa na wasiwasi wa kusalitiwa na mpenzi wako jambo ambalo huwa linazua mitafaruku kwa wapenzi na kusababisha kuchukizana na pengine kupelekea kuachana kabisa.


Kwahiyo nawashauri sana ndugu zangu mjitahidi kuepuka mambo kama haya ili kudumisha penzi zaidi.Sasa tujadiliane kuhusu suala hili na pia napenda kuuliza Je, penzi ni nini?