Tuesday, March 15, 2011

Si Kila Mshauri wa Mapenzi Anajua Kupenda........


SIKU moja nilikuwa katika shughuri zangu za kutoa ushauri katika suala zima la mapenzi na uhusiano katika ofisi zetu zilizoko Kiwani Bombom kijiwe Samli jijini Dar es Salaam, nilisikitika  kumuona mama mmoja akifika katika ofisi zetu huku akitokwa na machozi, yaani nilisikitika sana, sana na tena sana kwani nilipatwa na roro ya huruma.

Baada ya kuingia mama huyo alinieleza kuwa anataka ushauri juu ya mume wake kwani huyo mume wake huwa anamunyanyasa sana na kilichomfanya aje kwangu huku akitokwa na machozi ni kwa sababu mume wake alimutukana na kumwambia aondoke aende kwao. Mume wake huyo alimutaka achukue gari mbili nyumba moja, na kiwanja kilichoko Kigamboni lakini mwanamke huyo hakutaka kuondoka kwa mume wake kwani  bado anampenda sana na anamuhitaji sana na ndio maana anataka nimupe ushauri.

Nilimpa dozi kubwa ya ushauri jinsi ya kumrekebisha mwanaume mkorofi na kuwa baba mzuri mwenye upendo na familia yake. Nilimshauri mambo mengi juu ya kudumisha ndoa yake na nikamuhakikishia kuwa iwapo atafuata ushauri wangu hakika hatajutia kuja kwangu. Baada ya kumshauri sana mama huyo nilimuona kajawa na roho ya furaha sana, huzuni na majonzi aliyokuja nayo yalitoweka kama upepo na kuniona mimi kama ni mtu niliyebarikiwa na Mungu kwa kujua kushauri watu.

Mama wa watu alijikuta akinitamukia "Hakika wewe ni baba uliyejaa upendo kwa kila mtu na ninaamini mke wako anaishi kwa amani na raha tele hata kama huna pesa nyingi kama mume wangu kwani maneno yako ni matamu sana yanajenga na yanaleta amani ndani ya ndoa" aliniambia mama huyo na kuongeza  "Ukimwambia mwanamke yeyote aliyekamilika hakika yanamfariji sana, ndio maana ninakuambia kwamba wapo wanaume kama nyinyi wenye kujua upendo na ndoa ni nini? wewe ni baba pekee katika ulimwengu huu" alisisitiza mama huyo.


Lakini aliponiambia hayo nilisimama na kuvua koti langu na kuliweka katika hangs na pia nikakaa katika kiti changu, nikamtazama kwa macho ya huruma na kumtamkia kwamba mimi siyo najua kila kitu mimi ni binadamu kama wanaume wengine na ninamapungufu mengi tu, siyo tu katika maisha pia na hata katika masuala ya mapenzi na mahusiano. Kwahiyo sio kila mwanasaikolojia wa mapenzi anajua kupenda. Sasa tujadili juu ya jambo hili, Yasinta dada  yangu, Marcus kijana mpotevu, Koero mtaalam, Simon mchapakazi NK.