Tuesday, February 17, 2009

Maswali

NILIKUWA nimekabiliwa na majukumu mengi sana paka ilinipelekea kuwa nashinda njaa bila kunywa hata kahawa yetu ya kila siku ila sasa nimesimama tena ili kuweza kutafuna sawasawa hiki chakula chetu cha kila siku (kublogu) ila leo nitakuja na maswali ambayo yananiumiza kichwa kila siku.

1) Kupenda ni nini? na nini maana ya kupenda?
2)Ikiishi bila kuoa au kuolewa kuna hasara gani?
3)Kufanya tendo la ndoa maana yake nini?
4)Uzuri ni nini na ubaya ni nini?
5) Roho nzuri ni nini?

Haya ni hayo tu ndugu zangu ninaumia kichwa sana kutafakari juu ya maana ya maswali hayo ila nawaombeni tuchangie mambo haya katika kuyapatia maana yake. Amani kwako Markus, dada Yasinta, dada Koero, Fadhy na wengine wote na natumai tuko pamoja daima.