Sunday, May 17, 2009

Falsafa na Penzi


NIMERUDI tena ndugu zangu nilikuwa masomoni kwa muda kidogo ila sasa hivi niko kazini kwangu ninachati na mhariri wangu wa habari ambaye ndiye Mwalimu wangu Mkuu katika kuhakikisha jamii inaelimika kupitia vyombo mbalimbali vya habari.
Huko masomoni nimejifunza mambo mengi sana nimejifunza kuwa kumbe watanzania waliowengi hawajui kingereza!!!! Nilishaangaa sana Mhadhiri wangu wa lugha aliponiambia hata Kenya hawajui kingereza!!
Kwa sababu fani yangu ni Kudadisi nilimhoji kwa nini anasema hivyo ? Jibu alilonipa Ahhh!!! eti katika vitabu alivyosoma hakuna sehemu ambayo amekuta kumeandikwa rafudhi ya kingereza ya Afrika Mashariki!!(East African Accent) hayo yote nimejifunza kwa sababu nilikuwa nafuatilia kwa ukaribu sana mongozi wa lugha hii ya kingereza.
Ama kweli elmu haina Mwisho kwani nilijifunza mengi sana? Ikiwa pamoja na Mhadhiri wangu wa Falsafa alinifundisha kuwa elimu haina Mwisho huku akisema elimu inaanzia mtu anapozaliwa na pale anapokufa!!. Kwasababu napenda Falsafa niliamua kuziunganisha falsafa za Mhadhiri wangu na kuzifanyia kazi.
Jambo nililogundua ni kwamba hata penzi halina mwisho pendo linadumu siku zote ila kunakumchukia mtu fulani, lakini pia ukimchukia huyu utampenda huyu ndiyo maisha ya binadamu. Je kama tusingekuwa na upendo tungeishije katika dunia hii? Sasa tujadiliane ndugu zangu.




7 comments:

Yasinta Ngonyani said...

Kwanza nasema karibu tena kwani ulikuwa umepotea sana umekumbukwa sana. na hongera kwa kuongeza elimu

Fita Lutonja said...

Asante dada yangu Yasinta nimerudi katika kibaraza chetu ili tushirikiane katika kujenga na kupambanua hoja mbalimbali.

Fita Lutonja said...

Koero, Marcus na wengine natumai tuko pamoja nitafurahi zaidi nikijifunza kutoka kwenu katika mjadara wetu wa uandishi huria.

chib said...

Kutembea ni kuona mengi na kujifunza mengi pia.
Kuna waingereza ambao nao hawajui kiingereza vizuri pamoja na kuwa wamezaliwa na kukulia Uingereza, wanazungumza zaidi lugha ya mtaani. Watangazaji wa BBC kutoka uingereza, hulazimika kwenda kozi ya kiingereza ili watangaze kwa ufanisi zaidi. Usishangae sana ndugu yangu. Kuna baadhi ya watu hushangaa kuona au kusikia kuna watanzania wasiojua kiswahili, nafikiri utakubaliana nami. Ebu jaribu kuingia umasaini kwa utafiti wa haraka tu.

Fita Lutonja said...

Chib hayo yote nakubaliana na wewe kweli kuna watanazania ambao hawajui kiswahili tena wengi tu.
asante kwa maoni yako.

Albert Kissima said...

Kaka Fita naamini kisomo ulichokipata si kwa manufaa yako tu bali kwa manufaa ya jamii nzima, hivyo mimi na wanajamii kwa ujumla akili zetu zipo tayari kabisa kujifunza mengi kutoka kwako.
Karibu sana.

Fita Lutonja said...

Asante kaka kwa maoni mazuri sana uliyonipa ni kweli kabisa elimu niliyoipata ni kwa ajili ya jamii.

kwakweli nashukuru sana nakutakia siku njema na mungu akubariki sana.