Watu wengi hutoa machozi pale wanapoachwa na wapenzi wao, Mpenzi msomaji wa blogu yako uipendayo ya saikolojia leo nitakueleza kuhusiana na chozi la penzi: Unajua wataalamu wa mambo ya mapenzi wanasema kuwa Mwanamke ni mwepesi sana kutoa machozi pindi anapoachwa na mpenzi wake hii inatokana na mwanamke kuubwa na moyo wa kuwa na penzi la rohoni.
Wataalamu wa mambo ya mahaba wanasema kuwa wanawake wameumbwa kwa penzi la rohoni yaani la ndani tofauti na wanaume, hii ndiyo inasababisha mwanake akiachwa na mpenzi wake hujisikia vibaya na kujiona kama hafai kabisa kwa mwanaume yoyote kitendo ambacho kinamfanya anatoa machozi kwa wingi sana.
Mwanaume kaumbwa kwa penzi la fikra kama wanavyotufahamisha wataalamu wa mapenzi hii ndiyo maana wanaume wengi ni vigumu sana kulia pale wanapoachwa na wapenzi wao japo wapo wanaolia lakini sio wengi japokuwa huwa wanaumia sana rohoni lakini kutokana na elementi walizoumbwa nazo inakuwa vigumu kutoa machozi. "Nakusihi uendelee kuburudika zaidi na blogu yako usisahau kutoa maoni"