Tuesday, April 26, 2011

WANABLOGU NAWATAKIA PASAKA NJEMA


WAPENDWA katika bwana nawatakia pasaka njema. Mimi imenikumbusha mwaka 2005 nilipoamua kuokoka na kumurudia Mungu wangu kwa nguvu zote. Ndugu zangu nakumbuka ilikuwa mwezi wa tatu mwaka wa 2005 nikiwa pale Morogoro nilipata ubatizo na kuanza kujiandaa na pasaka ila ninachokikumbuka zaidi wakati nikibatizswa na Mch Peter Denis ni pale aliponishika kichwani na kuanza kuniombea nikiwa katikati ya maji ghafra nilipatwa na nguvu furani nikajikuta nalia kwa nguvu watu wote walishutuka ila mchungaji alinifariji na kunitaka nimshukuru Mungu.

Mch Peter Denis baada ya kunifariji alinishika kichwani na kunizamisha majini nilipotoka majini nikajisikia nimezaliwa upya machozi ambayo nilikuwa nalia yakakauka na muchugaji akaniambia kwa maneno ya upendo "Asante Mwanangu Hakika Umebarikiwa" Kwakweli namkumbuka sana mchungaji wangu na Mungu amubariki sana katika kazi yake ya utumishi. Japo kwa sasa niko Da,r ila Mchungaji Peter Denis sitamsahau kwani alifungua ukurasa mpya wa maisha yangu.

Kwahiyo ndugu zangu yatupasa kumshukuru Mungu kwa kila jambo hasa katika siku hizi za sikuku za Yesu Kristo. Mungu awabariki sana wanablogu, na pia awape nguvu kwa kazi zenu, maoni yenu juu yangu yatabarikiwa pia. Ameni.

Tuesday, March 15, 2011

Si Kila Mshauri wa Mapenzi Anajua Kupenda........


SIKU moja nilikuwa katika shughuri zangu za kutoa ushauri katika suala zima la mapenzi na uhusiano katika ofisi zetu zilizoko Kiwani Bombom kijiwe Samli jijini Dar es Salaam, nilisikitika  kumuona mama mmoja akifika katika ofisi zetu huku akitokwa na machozi, yaani nilisikitika sana, sana na tena sana kwani nilipatwa na roro ya huruma.

Baada ya kuingia mama huyo alinieleza kuwa anataka ushauri juu ya mume wake kwani huyo mume wake huwa anamunyanyasa sana na kilichomfanya aje kwangu huku akitokwa na machozi ni kwa sababu mume wake alimutukana na kumwambia aondoke aende kwao. Mume wake huyo alimutaka achukue gari mbili nyumba moja, na kiwanja kilichoko Kigamboni lakini mwanamke huyo hakutaka kuondoka kwa mume wake kwani  bado anampenda sana na anamuhitaji sana na ndio maana anataka nimupe ushauri.

Nilimpa dozi kubwa ya ushauri jinsi ya kumrekebisha mwanaume mkorofi na kuwa baba mzuri mwenye upendo na familia yake. Nilimshauri mambo mengi juu ya kudumisha ndoa yake na nikamuhakikishia kuwa iwapo atafuata ushauri wangu hakika hatajutia kuja kwangu. Baada ya kumshauri sana mama huyo nilimuona kajawa na roho ya furaha sana, huzuni na majonzi aliyokuja nayo yalitoweka kama upepo na kuniona mimi kama ni mtu niliyebarikiwa na Mungu kwa kujua kushauri watu.

Mama wa watu alijikuta akinitamukia "Hakika wewe ni baba uliyejaa upendo kwa kila mtu na ninaamini mke wako anaishi kwa amani na raha tele hata kama huna pesa nyingi kama mume wangu kwani maneno yako ni matamu sana yanajenga na yanaleta amani ndani ya ndoa" aliniambia mama huyo na kuongeza  "Ukimwambia mwanamke yeyote aliyekamilika hakika yanamfariji sana, ndio maana ninakuambia kwamba wapo wanaume kama nyinyi wenye kujua upendo na ndoa ni nini? wewe ni baba pekee katika ulimwengu huu" alisisitiza mama huyo.


Lakini aliponiambia hayo nilisimama na kuvua koti langu na kuliweka katika hangs na pia nikakaa katika kiti changu, nikamtazama kwa macho ya huruma na kumtamkia kwamba mimi siyo najua kila kitu mimi ni binadamu kama wanaume wengine na ninamapungufu mengi tu, siyo tu katika maisha pia na hata katika masuala ya mapenzi na mahusiano. Kwahiyo sio kila mwanasaikolojia wa mapenzi anajua kupenda. Sasa tujadili juu ya jambo hili, Yasinta dada  yangu, Marcus kijana mpotevu, Koero mtaalam, Simon mchapakazi NK.

Tuesday, March 8, 2011

Kwanini Wanawake Warembo Hupenda Kuolewa na Wanaume Wenye Sura Mbaya????


WANAWAKE wengi waliowazuri wa sura huwa wanapenda kuolewa na wanaume wabaya wa sura. Hii inatokana na ukweli kwamba wanawake wenye sura nzuri hupenda kuolewa na wanaume wenye sura mbaya ili kulinda uzuri wao kwani wanaamini kuwa iwapo ataolewa na mwanaume mwenye sura nzuri, uzuri wake hautaonekana kwa watu kwani mwanaume pia ataonekana mzuri jambo ambalo litamupunguzia mwanamke kuonekana mzuri katika jamii. Hii ndio maana wanawake wengi wenye sura nzuri wanapenda kuolewa na wanaume wenye sura mbaya. Dr. Linda Mtaalamu wa masuala ya mapenzi na uhusiano anasema " Wanawake wengi wenye sura nzuri wanatabia ya kutaka waonekane kuwa ni warembo, jambo ambalo linawapelekea kuolewa na wanaume wenye sura mbaya ili waendelee kushine katika jamii".

Pia wanaume wenye sura mbaya wanapenda kuoa wanawake wenye sura nzuri ili kulinda hishima yao kwa kupitia  wake zao. Kwahili ndugu msomaji naomba ujaribu kufanya uchunguzi wa kina kwa kuangalia wanaume wenye sura mbaya, utagundua kuwa wengi wao wanapenda kuoa wanawake wazuri na wengi wao tayari wameshaoa wanawake warembo. Je, kwa upande wa wanawake weusi; je, wanapenda wanaume wa aina gani? Na kwa upande wa wanaume weusi pia wanapenda wanawake wa aina gani? Pia na wewe kama unajitabua kuwa uko hivi au vile je, unapenda sweetheart wako aweje. Sasa tujadili.........................!!!!!

Tabia za Mwanamke


LEO nitaongelea kuhusiana na tabia za mwanamke. Tabia za mwanamke hasa katika suala zima la mapenzi ni kwamba mwanamke ni kiumbe kilichoumbwa kwa namna tofauti kabisa, kwani anauwezo mkubwa sana wa kumtambua mwanaume muongo au laghai wa mapenzi pia mwanamke ni binadamu aliyemvumilivu sana hasa akijua kuwa mume wake ni mwaminifu kwake kwa hili nakuoma Ndg. msomaji ebu jaribu kufanya  uchunguzi juu ya jambo hili.

Pia mwanamke katika mapenzi au ndoa huwa ni binadamu aneyependa sana kufarijiwa na kupewa pole kwa kila kitu ambacho kinaonekana kimemuumiza. Mwanasaikolojia mtaalamu wa masula ya mapenzi Dr. Linda wa chuo kikuu cha Havard nchini Marekani aliwahi kusema "Female needs to be satisfied by Male in each and every things" Kwa mujibu wa Linda mwanamke ni kiumbe kinachohitaji kurizishwa kwa kila kitu, kwa hiyo ndugu zangu inawapasa kuhakikisha unamurizisha mkeo ili  kujenga penzi la kudumu.

Monday, March 7, 2011

Wanablugu Nimerudi Tena

NIMERUDI tena baada ya kutingwa na kazi nyingi sana! Ila kwa sasa nimerudi kwenye chakula chetu cha kila siku nilikimis sana nilikuwa nakosa nguvu kwa sababu ya kukosa chakula chetu kwa wale ambao wanataka kujua nilikuwa wapi? Nilikuwa nimebanwa na jamaa mmoja anayeitwa muda hakika nilikuwa mutumwa wa muda kila kitu huyu muda alikuwa ananiamulisha! lo! Nimekoma na huyu muda!Hakiaka angekuwa anaonekana ningemkomoa kwelikweli! Ila nawapenda wote wanablogu wenzangu mmmwaaaaaa!!