Tuesday, March 8, 2011
Tabia za Mwanamke
LEO nitaongelea kuhusiana na tabia za mwanamke. Tabia za mwanamke hasa katika suala zima la mapenzi ni kwamba mwanamke ni kiumbe kilichoumbwa kwa namna tofauti kabisa, kwani anauwezo mkubwa sana wa kumtambua mwanaume muongo au laghai wa mapenzi pia mwanamke ni binadamu aliyemvumilivu sana hasa akijua kuwa mume wake ni mwaminifu kwake kwa hili nakuoma Ndg. msomaji ebu jaribu kufanya uchunguzi juu ya jambo hili.
Pia mwanamke katika mapenzi au ndoa huwa ni binadamu aneyependa sana kufarijiwa na kupewa pole kwa kila kitu ambacho kinaonekana kimemuumiza. Mwanasaikolojia mtaalamu wa masula ya mapenzi Dr. Linda wa chuo kikuu cha Havard nchini Marekani aliwahi kusema "Female needs to be satisfied by Male in each and every things" Kwa mujibu wa Linda mwanamke ni kiumbe kinachohitaji kurizishwa kwa kila kitu, kwa hiyo ndugu zangu inawapasa kuhakikisha unamurizisha mkeo ili kujenga penzi la kudumu.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
2 comments:
Umenena kaka!
Its true ndg yng
Post a Comment