Thursday, May 21, 2009

Mwingine anapenda wachaga wengine wasukuma


BINADAMU wote ni sawa lakini tunatofautiana kimawazo, fikra, kiutendaji, kipawa nk. Haya nilikuja kuyadhitisha katika kufuatilia fikra za Mwanafalsafa aliyekuwa maarufu sana kwa uchambuzi wa fikra na mawazo ambaye alikuwa anaitwa Plato.
Katika kazi yake ya "Republic" Plato alisema kuwa kila binadamu ameubwa tofauti kutokana na wengine kuwa na akili nyingi ambaye yeye aliwaita "golden boy" ambao yeye hawa aliwaelezea kuwa ni wale wanaweza kuwa viongozi wa nchi yaani (Philosphers, Gvern Planners and Rulers)

Wengine wanaakili ya kawaida "Silver boy" kwa mujibu wa Plato hawa ni wale wanaotakiwa kuwa walinzi wa nchi yaani askali jeshi na polisi pia alisema kundi la mwisho wa wale ambao wanaakili finyu "Iron Boy "hawa Plato alisema kuwa kwa kuwa wanauwezo mdogo wa kupambanua mambo kazi yao ni kulima na kuwa wazalishaji wa bidhaa za nchi.

Hii ilikuja pale nilipojaribu kufanya uchunguzi wangu na kugundua kuwa kumbe hata katika suala la upendo binadamu tuko tofauti wengine wanapenda wanene wengine wembamba na wengine weupe wengine weusi.

Katika makabira wengine wanapenda kabira fulani, kama mimi ninapenda wachaga na wengine hawapendi wachaga wengine wasomi wengine hawapendi wasiomi kwahiyo kutokana na hili binadamu tuko tofauti.

Je, katika mtazamo wako wewe unaona je? tujadili.

2 comments:

Masangu Matondo Nzuzullima (MMN) said...

Mhola? Kwa nini unapenda Wachaga? Tupeane siri bwana. Wasukuma wana matatizo gani???

Ni mara yangu ya kwanza kufika hapa na nimepapenda. Mimi huwa napenda kusoma vitabu mbalimbali vikiwemo vya wanasaikolojia na pengine hapa kwako nitakuwa nimepata njia ya mkato. Naona nitahamia!

Wabeja.

Unknown said...

SIFA ZA WACHAGA: Labda rangi wengi ni weupe, au wengi ni waasiriamali waziri. Pia hawachezei elimu au kazi, .Hata wakiiba/kufanysa maovu au utapeli wanasema "yesu wangu nisaidie". Na anawasaidia.