Sunday, November 21, 2010

Harufu ya Wizi Yanukia UDOM

Makamu mkuu wa  chuo Prof. Idrisa Kikula
LEO wapenzi wa blogu hii nitaongelea kidogo kuhusu wanafunzi wa chuo Kikuu cha Dodoma  (Udom), katika hali ya kushangaza na kusikitisha na pengine kupelekea kuathiri kisaikolojia katika hali ya kufikiri na kujiwekea malengo kwa wanafunzi hao.

Katika pitapita zangu kama mwandishi wa habari nilikutana na wanafunzi hao na waliponiona tu, wakanipokea kwa shangwe sana huku sura zao zikionyesha kupata furaha ya kuniona, nami kwa hali kama hiyo nilijikuta nawauliza kulikoni kisaikolojia wanaonekana kufadhaika sana?. Lakini kwa sura za huzuni wakanijibu.

"Kaka tunasikitishwa sana na harufu ya wizi inayotukabili katika chuo chetu" alisema Hamisi mwanafunzi wa mwaka wa tatu na kuongeza kuwa; "Harufu ya wizi inanuka hapa chuoni tunalazimishwa kulipa direct costs kubwa sana tofauti na miaka ya nyuma"

Wanafunzi hao waliendelea kusema kuwa mwaka huu wa masomo 2010/2011 wanalazimishwa kulipa direct costs jumla ya shilingi Tshs. 88,000/= kwa mhura, tofauti na mwaka wa masomo uliopita ambapo walilipa jumla ya Tshs. 76000/=

Walisema kutokana na kauli ya uongozi wa chuo hicho UDOSO waliwataka wasilipe pesa hizo bali walipe kiasi cha Tshs.81,000/= ambapo walichanganua kuwa accomodation ni Tshs. 56,000/= pesa ya mtihani ni Tshs. 20,000/= na hela ya usajiri ni Tshs. 5,000/= jumla Tshs. 81,000/=, lakina pamoja na tamko la UDOSO uongozi wa chuo bado unakataa, jambo ambalo linawasikitisha wanafunzi hao.

Walisema chuo kinatakiwa kutoa maelezo ya kutosha ili kuwalizisha wanafunzi hao kwani bila maelezo ya kutosha wanaona kama wanaibiwa pesa zao, na ukizingatia wengi wao wanatoka katika familia masikini sana .

Sasa ndugu wanablogu wenzagu sasa tujadili kuhusu chuo hicho kuwa na utaratibu usioeleweka kwa wanafuzni. Je, dalili gani hasa? Je, ni utaratibu mzuri unafanya na chuo chetu  kikuu Afrika mashariki na kati? Tatizo liko wapi kwa uongozi wa chuo au? Nakaribisha maoni yenu bonyeza katika kisantuku kilichoandikwa toa maoni na utoe maoni yako yatasomwa na watanzania dunia nzima.

3 comments:

Masangu Matondo Nzuzullima (MMN) said...
This comment has been removed by the author.
Masangu Matondo Nzuzullima (MMN) said...

Asante kwa makala haya. Wanafunzi hawa wameshajaribu kuwasiliana na uongozi wa chuo kupitia chama chao? Kama walishajaribu walipewa jibu gani? Uzoefu wangu unaonyesha kwamba kukimbilia kutoa malalamiko katika vyombo vya habari mara nyingi huwa siyo njia sahihi hasa ikifanywa kwa kukurupuka.

Kwa upande mwingine, ni nani anayewalipia hizi hela zote? Wanapata mikopo kutoka serikalini au wanajisomesha? Bila mikopo nadhani mtoto wa mkulima wa kawaida ninayemfahamu kutoka kule Usukumani kamwe hataweza kusoma. Siku tutakapokuja kufuta hii mikopo basi itabidi tuwe na utaratibu mbadala mzuri. Vinginevyo masikini watakuwa wanaisikia elimu ya juu kwenye bomba tu!

UDOM nasikia inasifika kwa udini. Bila kuwa muumini wa dini fulani hivi kabisa huwezi kupata ajira hapo na hata ukiipata basi hutaenda popote. Kama hii ni kweli basi ni jambo la kusikitisha!

Fita Lutonja said...

Asante sana kaka Masangu kwa maoni yako mazuri nilijaribu kufanya follow up nikapata habari za kuaminika kuwa ni kweli Udom kunaubaguzi wa dini waisilamu wanapata favour zaidi ya wakristo lakini katika kutabiri kwangu kama mwandishi wa habari ninasema kuwa chuo hicho hakitafika mbali