Tuesday, March 8, 2011
Kwanini Wanawake Warembo Hupenda Kuolewa na Wanaume Wenye Sura Mbaya????
WANAWAKE wengi waliowazuri wa sura huwa wanapenda kuolewa na wanaume wabaya wa sura. Hii inatokana na ukweli kwamba wanawake wenye sura nzuri hupenda kuolewa na wanaume wenye sura mbaya ili kulinda uzuri wao kwani wanaamini kuwa iwapo ataolewa na mwanaume mwenye sura nzuri, uzuri wake hautaonekana kwa watu kwani mwanaume pia ataonekana mzuri jambo ambalo litamupunguzia mwanamke kuonekana mzuri katika jamii. Hii ndio maana wanawake wengi wenye sura nzuri wanapenda kuolewa na wanaume wenye sura mbaya. Dr. Linda Mtaalamu wa masuala ya mapenzi na uhusiano anasema " Wanawake wengi wenye sura nzuri wanatabia ya kutaka waonekane kuwa ni warembo, jambo ambalo linawapelekea kuolewa na wanaume wenye sura mbaya ili waendelee kushine katika jamii".
Pia wanaume wenye sura mbaya wanapenda kuoa wanawake wenye sura nzuri ili kulinda hishima yao kwa kupitia wake zao. Kwahili ndugu msomaji naomba ujaribu kufanya uchunguzi wa kina kwa kuangalia wanaume wenye sura mbaya, utagundua kuwa wengi wao wanapenda kuoa wanawake wazuri na wengi wao tayari wameshaoa wanawake warembo. Je, kwa upande wa wanawake weusi; je, wanapenda wanaume wa aina gani? Na kwa upande wa wanaume weusi pia wanapenda wanawake wa aina gani? Pia na wewe kama unajitabua kuwa uko hivi au vile je, unapenda sweetheart wako aweje. Sasa tujadili.........................!!!!!
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
10 comments:
Wanaume nao kwa upande wao....
http://matondo.blogspot.com/2010/10/utafiti-wanaume-huvutiwa-zaidi-na-sura.html
Hii kitu sio rahisi kihivyo kwa kuwa naamini swala la uzuri na ubaya sio rahisi kihivyo kitu kifanyacho nishashuhudia mwenyewe anikiringiwa na mtu ambaye matamanio ni ziro ingawa anajiamini namtamani !
Naamini hii kitu ni ngumu kuirahisisha kihivyo!
Ni mtazamo tu wangu!
Ok asanteni sana kwa maoni yenu mazuri
Kwa ajili asimuonee wivu mume wake kwa wanawake wengine.
Aaaaah! Kaka Lutonja hapa sikubaliani na wewe kabisaa labda utupe mifano halisi..
Asante kwa mada motomoto..
Uzuri wa mtu anaujua mtu,kwani mzuri kwako kwa mwingine si mzuri!inategemea wewe umependea mguu wake na Kitururu kapendea nywele!.
me ninachojua uzur na ubaya wa mtu upo machon kwa mtu, kwahyo wewe unaweza kumuona huyu mtu kama mbaya lakin mwenzio anaona kawaida au mzuri sana
Nadhani kwa Upande wa Mwanamke nzuri anapo olewa na Mwanamume ambaye sio nzuri, mara nyingi hufuata HELA na si tu kutaka uzuri wake uendelee kuonekana ILA kwa Mwanamume huaga tofauti kidogo mara nyingi Mwanamume hupenda kuwa na mwanamke nzuri kwa ajili tu ya kujionyesha na kujipatia sifa kwa Rafiki zake na hata jamii kwa ujumla. na mara nyengine ni KUAMINI kuwa mwanamke nzuri atakuzalia watoto wazuri watakao kupa hadhi kwa kupata waume wenye hea.
Kazi ya Mungu ni njema ktk uumbaji. Hakuna makosa wala mapungufu ktk kazi yake ya kumuumba mwanadamu, hata yule aliyezaliwa kilema ni ni ili kazi/uweza wake upate kudhihirika. Kwa ww uliyeumbwa,(mwanadamu) Mungu hakupi vyote na pia hakunyimi vyote, hivyo basi ridhika na jikubali jinsi ulivyo na mshukuru MUNGU.
Habari hii binafsi naona kama wanawake wazuri wapo special kwa kupiga pesa kwani uzuri wa mwanaume kwao sio kigezo katika maisha yao.
Post a Comment