Tuesday, March 15, 2011

Si Kila Mshauri wa Mapenzi Anajua Kupenda........


SIKU moja nilikuwa katika shughuri zangu za kutoa ushauri katika suala zima la mapenzi na uhusiano katika ofisi zetu zilizoko Kiwani Bombom kijiwe Samli jijini Dar es Salaam, nilisikitika  kumuona mama mmoja akifika katika ofisi zetu huku akitokwa na machozi, yaani nilisikitika sana, sana na tena sana kwani nilipatwa na roro ya huruma.

Baada ya kuingia mama huyo alinieleza kuwa anataka ushauri juu ya mume wake kwani huyo mume wake huwa anamunyanyasa sana na kilichomfanya aje kwangu huku akitokwa na machozi ni kwa sababu mume wake alimutukana na kumwambia aondoke aende kwao. Mume wake huyo alimutaka achukue gari mbili nyumba moja, na kiwanja kilichoko Kigamboni lakini mwanamke huyo hakutaka kuondoka kwa mume wake kwani  bado anampenda sana na anamuhitaji sana na ndio maana anataka nimupe ushauri.

Nilimpa dozi kubwa ya ushauri jinsi ya kumrekebisha mwanaume mkorofi na kuwa baba mzuri mwenye upendo na familia yake. Nilimshauri mambo mengi juu ya kudumisha ndoa yake na nikamuhakikishia kuwa iwapo atafuata ushauri wangu hakika hatajutia kuja kwangu. Baada ya kumshauri sana mama huyo nilimuona kajawa na roho ya furaha sana, huzuni na majonzi aliyokuja nayo yalitoweka kama upepo na kuniona mimi kama ni mtu niliyebarikiwa na Mungu kwa kujua kushauri watu.

Mama wa watu alijikuta akinitamukia "Hakika wewe ni baba uliyejaa upendo kwa kila mtu na ninaamini mke wako anaishi kwa amani na raha tele hata kama huna pesa nyingi kama mume wangu kwani maneno yako ni matamu sana yanajenga na yanaleta amani ndani ya ndoa" aliniambia mama huyo na kuongeza  "Ukimwambia mwanamke yeyote aliyekamilika hakika yanamfariji sana, ndio maana ninakuambia kwamba wapo wanaume kama nyinyi wenye kujua upendo na ndoa ni nini? wewe ni baba pekee katika ulimwengu huu" alisisitiza mama huyo.


Lakini aliponiambia hayo nilisimama na kuvua koti langu na kuliweka katika hangs na pia nikakaa katika kiti changu, nikamtazama kwa macho ya huruma na kumtamkia kwamba mimi siyo najua kila kitu mimi ni binadamu kama wanaume wengine na ninamapungufu mengi tu, siyo tu katika maisha pia na hata katika masuala ya mapenzi na mahusiano. Kwahiyo sio kila mwanasaikolojia wa mapenzi anajua kupenda. Sasa tujadili juu ya jambo hili, Yasinta dada  yangu, Marcus kijana mpotevu, Koero mtaalam, Simon mchapakazi NK.

11 comments:

Yasinta Ngonyani said...

Ni mjadala mzuri...wanaume kama huyu wapo wengi tu na sio wanaume tu kuna wanawake pia ambao wanafikiri kupenda/kumpenda mtu ni kwasababu ni TAJIRI. Lakini mimi binfsi nawapinga kabisa kwanyi hilop si penzi kabisa. Kwasababu kama unampenda mtu kwa mali aliyo nayo maana yake unapenda mali yake si mtu mwenyewe. Nampongeza huyo mama kwani hawapo akina mama kama hawa wengi ambao wanakataa magari,nyumba nk.

Na kuhusu kutoa ushauri katika mapenzi ni kweli si kila mshauri anajua kupenda. Kuna washauri wengine wanaweza kuwashauri wengine wakati yeye mwenyewe huko nyumbani ni vurumai tu. Na kuna wengine ni kweli wanakuwa washauri wazuri na pia wanapenda kweli. mmmhh naacha na wengine waseme....

Fita Lutonja said...

Dada Yasinta unabusara sana, unaakili sana kuzidi maelezo na ninafikiri unajua kupenda na kuishi na familia yako vizuri daima Mungu atakubariki sana dada yangu.

Umenena ya kweli kuwa utajili sio chanzo cha kumpenda mtu bali upendo unatokana na mvutano kati ya watu wawili.

Unknown said...

Changamoto ni nyingi na zipo wazi, ni sawa na kusema; mwimbaji wa nyimbo za injili ambaye ujumbe anaoutoa ni pamoja na watu kuacha uzinzi lakini yeye anazini.

Ninapotafakari mfumo wa maisha shetani aliotushinikizia nikilinganisha na kisa ulichokutana nacho katika kazi hii ya kushauri nagundua kuwa hata wanaosema watapambana na mafisad (ufisadi) ukiwafuatilia kwa makini sana utagundua nao wanafisadisha ila kwa namna ambayo huwezi gundua.

Nitolee mfano mwingine; mafundi ama ujenzi au capenter. Wanajenga nyumba nzuri sana ama kutengeneza makochi au makabati mazuri na ya kisasa lakini wao hivyo vitu kwao katika familia hakuna.

Hivyo wazo la kwamba si kila mshauri wa mapenzi anajua kupenda ni halisi kweli. Maana kuna waalimu wanafundisha uimbaji tena utafundishwa hadi utaimba vizuri katika hali na kiwango cha juu lakini huyo mwalimu yeye hawezi kuimba-umkimpa SOLO tu (lead) hata umeme unaweza zimika ghafla kutokana na sauti mbaya atakayoitoa.

Fita Lutonja said...

Macharia kaka yangu maoni yako ni poa kabisa nimefurahi sana kuyaona. Asante sana

Simon Kitururu said...

Inasemekana WALIMU wazuri mashuleni bado kwa kuwa ni WALIMU inamaana wao wenyewe wanayoyafundisha wanayajua kwa kuyafundisha tu la sivyo wangekuwa ni wafanyaji kivitendo.

Ndio maana unasikia mara nyingi mwalimu wa BIASHARA hukuti anafanya biashara.:-(

Ila mapenzi ni kitu kingine kabisa kwa kuwa unaambiwa MAPENZI kama IMANI mara nyingi apendaye sana kama AAMINIYE sana dawa za BABU pale loliondo,...
...ukimshauri mambo ya kutumia akili hata KUELEWA kwa kuwa kupenda na MAPENZI na kutumia akili haviendani.

Na kama unatumia akili kumpenda MTU au wakati unampenda mtu ,..
... labda huyo MTU hujampenda vizuri.


Na unaambiwa siri ya hata UKIMWI kuendelea kuenea sio kuwa watu hawaogopi UKIMWI ila pia kuna engo ya kupenda ambayo inafanya hata wahubirio matumizi ya condomu kujikuta kwa awazinguao kimapenzi wamekumbuka baada ya penzi kitendo kufanyika.:-(


Mimi naamini kila mshauri wa MAPENZI anajua KUPENDA ila pendo si kitu mtu kwa kutumia akili anauwezo wa kufikia kupewa shahada analijua hasa ukizingatia MAPENZI ,...
... labda ni aina ya ukichaa kidogo na kama unajua ufanyalo kuanzia A mpaka Z katika mapenzi labda wewe ufanyalo sio PENZI!

Ni wazo tu!

Fita Lutonja said...

Asante kwa maoni yako Simoni watazamaji na wasomaji wa blogu hii nzuri watayapata

Simon Kitururu said...

@Mkuu Fita : Lilikuwa ni wazo tu na sjui kwanini ningependa atakaye nisoma afikiriye kivyake!:-(

Mkuu Fita jumapili njema!

Fita Lutonja said...

Asante kakapia nami nakutakia jumapili njema natumai tuko pamoja mkuu

Simon Kitururu said...

Pamoja Sana Mkuu!

Masangu Matondo Nzuzullima (MMN) said...

Ni yale yale ya daktari anakushauri uache sigara kwa sababu zitakuua wakati huo huo mwenyewe anavuta....

Au pengine ni fuata nikwambialo lakini usifuate matendo yangu. Binadamu!

Fita Lutonja said...

ni kweli kabisa kaka matondo