Tuesday, December 9, 2008

Penzi halina Mzee


Nani alikuambia kuwa mzee hapendwi na vijana? nani alikuambia kuwa mzee hajui kuhondomola? nani alikuambia kuwa mzee hajui kuonyesha penzi la kweli? Katika dunia hii penzi ni kitu kizuri sana.


Kuna watu wengine wanasema mimi siwezi kuolewa na mzeee? na wengine mimi siwezi kuoa mtu ambaye ananizidi umri yote hayo ya nini? kwani penzi linazeeka? Penzi daima si la mzee wala kijana peke yake bali penzi ni la wote.


Kuna rafiki yangu mmoja wa kiume anahela za kawaida tu, na ana gari moja alinunuliwa na mpenzi wake, huyo rafiki yangu aliwahi kuniambia yeye habagui cha mwanamke mzee au msichana anachojali ni yule ambaye ana hela tu. Nilishanga sana nikajua rafiki yangu hana penzi la kweli kwa wanawake.


Ndugu kitu cha msingi ambacho ninataka nikueleze ni kwamba kama wewe umetokea kumpenda mtu ambaye ni mkubwa kuzidi wewe usimuache kwa kisingizio cha ukubwa bali uangaliwe penzi la kweli kama unampenda na yeye pia anakupenda basi yawapasa muoane na penzi lenu litadumu kwa sababu mnapendo la rohoni.

3 comments:

Yasinta Ngonyani said...

Fita ni kweli penzi halina mzee wala kijana na pengine hata watoto.

Karibu tena kwani ulipotea sana

MARKUS MPANGALA said...

Sasa dada Yasinta utaua BENDI jamani kweli penzi hata mtoto? ndiyo penzi halina mzee wala kijana sawa lakini UTAMU WAKE vipi? lakini ukipeda na kupendwa huoni hata nyoka!!!1 kunoga jamani mmmmmmm mpaka unamung'unya maneno

Fita Lutonja said...

Asante nimekaribia dada Yasinta kumbuka kuwa penzi ni kupenda kutoka rohoni