KARIBU tena ndugu zangu leo napenda kujua zaidi kuhusiana na mwananke wa kihidi na wakiafrika nani mzuri zaidi na nani anahusudu mapenzi kuliko. Kwani kumekuwepo na mkanganyiko wengine wanasema wahindi wanabaridi sana wengine wanasema waafirika wanajoto sana je, ni kweli? Wengine wafrika ni wazuri wengine wahindi ni wazuri. Sasa tujadili kupitia maoni yenu.
Thursday, May 21, 2009
Mwingine anapenda wachaga wengine wasukuma
BINADAMU wote ni sawa lakini tunatofautiana kimawazo, fikra, kiutendaji, kipawa nk. Haya nilikuja kuyadhitisha katika kufuatilia fikra za Mwanafalsafa aliyekuwa maarufu sana kwa uchambuzi wa fikra na mawazo ambaye alikuwa anaitwa Plato.
Katika kazi yake ya "Republic" Plato alisema kuwa kila binadamu ameubwa tofauti kutokana na wengine kuwa na akili nyingi ambaye yeye aliwaita "golden boy" ambao yeye hawa aliwaelezea kuwa ni wale wanaweza kuwa viongozi wa nchi yaani (Philosphers, Gvern Planners and Rulers)
Wengine wanaakili ya kawaida "Silver boy" kwa mujibu wa Plato hawa ni wale wanaotakiwa kuwa walinzi wa nchi yaani askali jeshi na polisi pia alisema kundi la mwisho wa wale ambao wanaakili finyu "Iron Boy "hawa Plato alisema kuwa kwa kuwa wanauwezo mdogo wa kupambanua mambo kazi yao ni kulima na kuwa wazalishaji wa bidhaa za nchi.
Hii ilikuja pale nilipojaribu kufanya uchunguzi wangu na kugundua kuwa kumbe hata katika suala la upendo binadamu tuko tofauti wengine wanapenda wanene wengine wembamba na wengine weupe wengine weusi.
Katika makabira wengine wanapenda kabira fulani, kama mimi ninapenda wachaga na wengine hawapendi wachaga wengine wasomi wengine hawapendi wasiomi kwahiyo kutokana na hili binadamu tuko tofauti.
Je, katika mtazamo wako wewe unaona je? tujadili.
Wednesday, May 20, 2009
Mwanafalsafa Socrates alihusudu ndoa
SIKU moja nilikuwa naelekea kwenye press conference moja tukiwa na rafiki yangu ambaye ni mwanahabari mwenzangu tulipofika maeneo ya Magomeni akaniambia kuwa anataka kuoa nami nikatafakari kwa kina maelezo kisha nikamjibu kuwa ni jambo jema kuoa kwani kuwa na mke ni mojawapo ya maisha tuliopangiwa na Mungu.
Mara nikakumbuka usemi wa Mwanafalsafa wa Kigiriki aitwaye Socrates naye alidhamini sana ndoa kwani aliwahi kusisitiza kuwa kama ukiona maisha ni magumu ni vizuri kuoa mwanamke Mzuri. "If you see life is hard you have to find a good wife to refresh your mind" alisema Socrates.
Jambo la kuwa na Mwanamke ni mhimu sana kwani watu wengi hasa katika nchi zinazoendelea huwa wanapata msongo wa mawazo kutokana na maisha kuwa magumu lakini Mwanasayansi Samuel Spire anasema kuwa kuwa na Mwanamke ni mojwapo ya kupunguza msongo huo wa mawazo.
Anasema kuwa mwanamke anasaidia kuondoa msogo wa mawazo kwa mwanaume vilevile mwanaume anasaidia kuondoa msongo wa mawazo kwa mwanamke. Hii inatokana na homoni zinazotolewa pindi mwanaume au mwanake anapokuwa na mpenzi wake.
Je , wewe ndungu yangu ulishawahi kukutana na msongo wa mawazo baadaye ulipomuona mpenzi wako ukajisikia uko fresh? sasa tujadili katika kibaradha chetu.
Sunday, May 17, 2009
Falsafa na Penzi
NIMERUDI tena ndugu zangu nilikuwa masomoni kwa muda kidogo ila sasa hivi niko kazini kwangu ninachati na mhariri wangu wa habari ambaye ndiye Mwalimu wangu Mkuu katika kuhakikisha jamii inaelimika kupitia vyombo mbalimbali vya habari.
Huko masomoni nimejifunza mambo mengi sana nimejifunza kuwa kumbe watanzania waliowengi hawajui kingereza!!!! Nilishaangaa sana Mhadhiri wangu wa lugha aliponiambia hata Kenya hawajui kingereza!!
Kwa sababu fani yangu ni Kudadisi nilimhoji kwa nini anasema hivyo ? Jibu alilonipa Ahhh!!! eti katika vitabu alivyosoma hakuna sehemu ambayo amekuta kumeandikwa rafudhi ya kingereza ya Afrika Mashariki!!(East African Accent) hayo yote nimejifunza kwa sababu nilikuwa nafuatilia kwa ukaribu sana mongozi wa lugha hii ya kingereza.
Ama kweli elmu haina Mwisho kwani nilijifunza mengi sana? Ikiwa pamoja na Mhadhiri wangu wa Falsafa alinifundisha kuwa elimu haina Mwisho huku akisema elimu inaanzia mtu anapozaliwa na pale anapokufa!!. Kwasababu napenda Falsafa niliamua kuziunganisha falsafa za Mhadhiri wangu na kuzifanyia kazi.
Jambo nililogundua ni kwamba hata penzi halina mwisho pendo linadumu siku zote ila kunakumchukia mtu fulani, lakini pia ukimchukia huyu utampenda huyu ndiyo maisha ya binadamu. Je kama tusingekuwa na upendo tungeishije katika dunia hii? Sasa tujadiliane ndugu zangu.
Tuesday, February 17, 2009
Maswali
NILIKUWA nimekabiliwa na majukumu mengi sana paka ilinipelekea kuwa nashinda njaa bila kunywa hata kahawa yetu ya kila siku ila sasa nimesimama tena ili kuweza kutafuna sawasawa hiki chakula chetu cha kila siku (kublogu) ila leo nitakuja na maswali ambayo yananiumiza kichwa kila siku.
1) Kupenda ni nini? na nini maana ya kupenda?
2)Ikiishi bila kuoa au kuolewa kuna hasara gani?
3)Kufanya tendo la ndoa maana yake nini?
4)Uzuri ni nini na ubaya ni nini?
5) Roho nzuri ni nini?
Haya ni hayo tu ndugu zangu ninaumia kichwa sana kutafakari juu ya maana ya maswali hayo ila nawaombeni tuchangie mambo haya katika kuyapatia maana yake. Amani kwako Markus, dada Yasinta, dada Koero, Fadhy na wengine wote na natumai tuko pamoja daima.
1) Kupenda ni nini? na nini maana ya kupenda?
2)Ikiishi bila kuoa au kuolewa kuna hasara gani?
3)Kufanya tendo la ndoa maana yake nini?
4)Uzuri ni nini na ubaya ni nini?
5) Roho nzuri ni nini?
Haya ni hayo tu ndugu zangu ninaumia kichwa sana kutafakari juu ya maana ya maswali hayo ila nawaombeni tuchangie mambo haya katika kuyapatia maana yake. Amani kwako Markus, dada Yasinta, dada Koero, Fadhy na wengine wote na natumai tuko pamoja daima.
Saturday, January 3, 2009
Nilimpenda kwa sababu....?
KATIKA kumpenda mtu huwa kunachangiwa na vitu vingi sana kwa sababu binadamu tunatofautiana kifikra, kimaumbile, kimutazamo, kiuelewa, kihisia n.k. ambayo yote haya katika mapenzi huchangia mwamsho (feelings) wa mwili.
Kutokana vitu vyote hivyo binadamu anaweza kumpenda mtu mweusi, mweupa, mfupi, mwembamba, mnene nk.
Kuna watu wanapenda kuwa na wapenzi wembamba yaani watu hawa wakiona mwanamke/mwanaume mwembamba huwa wanapata hisia kubwa sana ya kumpenda na kutamani kufanya nae mapenzi ili walidhike kuwa wamehondomola kifaa ambacho wanakipenda sana.
Wengine wakiwaona mtu mnene hupata mwamsho wa kutaka kumuhondomola ili kulidhika kuwa wamefanya na mtu ambaye ni mzuri. Si mapenzi hata kuoa kunatokana na sababu hizo za kupata hisia ya yule umpendae hasa kukuvutia kwa jinsi alivyo.
Mwanasaikolojia na Mchungaji, Hoven Michal wa chuo kikuu cha Wheaton School of Thelogy katika jimbo la texas nchini Marekani alibainisha katika utafiti wake juu ya hisia kwa binadamu aliuandikia kitabu ambacho alikiita kwa jina la "Feeligs & Love" ya kwamba matendo ya mahaba kwa binadamu yanatawaliwa na hisia hasa kwa yule anayekuvuti.
Naye Fredy Hasin wa Dar es Salaam aliwahi kusimulia kuwa alimpenda sana mama Suzy (mke wake) na alikuwa anamhondomola vizuri sana wakati wa chakula cha usiku lakini alikuja kumchukia kutokana na kunenepa ghafra jambo ambalo alikuwa halitaki katika maisha yake.
Pia Maganga Magembe ambaye ni askali polisi wa kituo kidogo cha Nyakato aliwahi kuahadithia kuwa yeye anapenda wanawake wanene kwa sababu huwa anapata nafasi nzuri ya kufaidi tunda tamu wakati wa chakula cha usiku, jambo ambalo linampelekea kujiona fahari katika dunia ya maopenzi.
Sayuni Mahina alipohojiwa na Mwandishi Huria wa blogu hii alidhibitisha kuwa yeye mme wake ni Mwembamba na anapenda wanaume wa aina hiyo kwa sababu huwa wanamhondomola vizuri sana na kumfanya ajisikie utamu hadi kwenye kichwa. "Utamu huu ambao huwa naupata sijawahi kuupata sijui Mungu aliutoa wapi?" alihoji mama huyo.
Je, Mpenzi wa blogu hii wewe unapenda wako penzi wa aina gani? Sasa tujadiliane mada hii niliwahi kudika kipindi cha nyuma.
Friday, January 2, 2009
Nimefurahi sana
Haya ndugu zangu napenda kuwaarifu kitu ambacho ninataka kukifanya kwa sasa hivi. Kitu hicho ni kwamba nataka kwenda kusoma chuo kwani wahenga walituambia ya kwamba "Elimu Haina Mwisho" na kitabu kitakatifu kinatuambia ya kuwa "Mshikeni Elimu Msimuache aende zake maana huyo ni uzima wetu" kwahiyo wanablogu wenzangu nataka niendelee kufuata haya maandiko ili nione kama yanaukweli.
Ila ninatumai tuko pamoja popote nitakapokuwa, Bwaya, Markus mpangala, Dada Yasinta, Da Koero, na wengine Mungu awabariki sana.
Subscribe to:
Posts (Atom)