Friday, January 2, 2009

Nimefurahi sana


Haya ndugu zangu napenda kuwaarifu kitu ambacho ninataka kukifanya kwa sasa hivi. Kitu hicho ni kwamba nataka kwenda kusoma chuo kwani wahenga walituambia ya kwamba "Elimu Haina Mwisho" na kitabu kitakatifu kinatuambia ya kuwa "Mshikeni Elimu Msimuache aende zake maana huyo ni uzima wetu" kwahiyo wanablogu wenzangu nataka niendelee kufuata haya maandiko ili nione kama yanaukweli.


Ila ninatumai tuko pamoja popote nitakapokuwa, Bwaya, Markus mpangala, Dada Yasinta, Da Koero, na wengine Mungu awabariki sana.

6 comments:

John Mwaipopo said...

washa moto nenda kwa spidi 160 mpaka huko shule. ila usitusahau na usisahau kahawa tuliyokuwa tukinywa wote.

Fita Lutonja said...

Haya asante sana kaka Mwaipopo kublogu ninajua kuwa ni chai yetu kamwe sitasahau hata kidogo.

MARKUS MPANGALA said...

Duuh mkuu! poleni kwa Cluster yenu kucheleweshwa lakini naamini sababu zilizotolewa zilikuwa za msingi sana. Lakini hata hivyo NAKUONYA ukifanya kosa la kutoblogu mwanawane mashtaka yapo palepale, hakika SITANII. ha ha ha najua tarehe ya kwenda chuo bado ipo ipo kwanza au vipi mzee mwenyewe, kwahiyo fanya mambo basi. tupatie mada zako za MAHABA NA MAPENZI KOTOMOTO.

Duuh dada Yasinta anakunywa ULANZI na kumbikumbi, hapo bado hajanywa myakaya.

Kila la heri kwa elimu nami pamoja na suluba za hapa na pale kilimani mlimani TUNAKOMAA nao tena tena nabashiri mgomo ujao ni mkubwa kupindukia. nabashiri hivyo kwani ninajua dalili zake.

amani iwe nasi, upendo uwe nasi

Fita Lutonja said...

Dada Yasinta naona kweli anajinafasi kwa sasa, ila ni jambo jema.

Pamoja na kwamba ninaondoka kwenda masomoni nawahakikisheni wanablogu ya kwamba mimi kublogu ni sawa na chai yangu.

Markus nafurahi sana kuwa pamoja ila nimesahau kitu kimoja naomba munikumbushie siku ya blogu duniani ni tarehe ngapi?

MARKUS MPANGALA said...

Duu ngoja nimuulize BWAYA anajua sana hilo, nadhani 18 novemba kama sikosei. ebu kwanza tumbipu basi pengine atapiga haya anza basioiiii

Fita Lutonja said...

Haya bwana habari ndio hiyo nimefurahi kwelikweli