Tuesday, April 26, 2011
WANABLOGU NAWATAKIA PASAKA NJEMA
WAPENDWA katika bwana nawatakia pasaka njema. Mimi imenikumbusha mwaka 2005 nilipoamua kuokoka na kumurudia Mungu wangu kwa nguvu zote. Ndugu zangu nakumbuka ilikuwa mwezi wa tatu mwaka wa 2005 nikiwa pale Morogoro nilipata ubatizo na kuanza kujiandaa na pasaka ila ninachokikumbuka zaidi wakati nikibatizswa na Mch Peter Denis ni pale aliponishika kichwani na kuanza kuniombea nikiwa katikati ya maji ghafra nilipatwa na nguvu furani nikajikuta nalia kwa nguvu watu wote walishutuka ila mchungaji alinifariji na kunitaka nimshukuru Mungu.
Mch Peter Denis baada ya kunifariji alinishika kichwani na kunizamisha majini nilipotoka majini nikajisikia nimezaliwa upya machozi ambayo nilikuwa nalia yakakauka na muchugaji akaniambia kwa maneno ya upendo "Asante Mwanangu Hakika Umebarikiwa" Kwakweli namkumbuka sana mchungaji wangu na Mungu amubariki sana katika kazi yake ya utumishi. Japo kwa sasa niko Da,r ila Mchungaji Peter Denis sitamsahau kwani alifungua ukurasa mpya wa maisha yangu.
Kwahiyo ndugu zangu yatupasa kumshukuru Mungu kwa kila jambo hasa katika siku hizi za sikuku za Yesu Kristo. Mungu awabariki sana wanablogu, na pia awape nguvu kwa kazi zenu, maoni yenu juu yangu yatabarikiwa pia. Ameni.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
6 comments:
Mwendelezo wa pasaka njema uwe nawe pia...Mungu ni muweza
Asante kwa maoni mazuri ubarikiwe
Kwako pia Mkuu Pasaka njema!
asante mkuu simon nafurahi kuona tuko pamoja
Duh! umepotea kwelikweli? upo mzima/salama?
Karibu tena mkuu
Post a Comment