Wednesday, March 28, 2012

JAMANI NIMERUDI TENA NILIKUWA MASOMONI

IMERUDI tena kwenye kibaraza chetu, karibuni sana nilikuwa nigeria nasoma masters ya Journalism Curriculum Development and Designing nimemaliza nimerudi TZ  coz naipenda nchi yangu japo mafisadi wananikatisha tamaa mpaka nilifikia uamuzi wa kutaka nisirudi TZ lakin rafiki yangu mpendwa Cretus  akanishauri nirudi nimefurahi kukutana na watanzania wenzangu. Hapo juu ni dada ambaye alinisaidia kuchapa RESEARCH REPORT yangu, ni dada mkarim sana hakika sitamsahau ktk maisha yangu, bila yeye yawezekana nisingemaliza masomo yangu.

Jamani nimekumbuka kitu kimoja niliambiwa na rafiki yangu ambaye tulikuwa tunasoma naye huko nje aliniambia "Tanzania ni nchi nzuri sana lakini kuna ufisadi mkuu katika sekta ya elimu hasa wanapoajiriwa walimu wapya kwani huwa hawalipwi mishahara yao miezi miwili kitu ambacho kinawafanya waishi maisha ya kuomba omba kwa wanafunzi na walimu wengine" maneno haya yalitia uchungu sana na nchi yangu. Ni hayo tu ila nawaomba tujadiri "JE NCHI YETU INATOA HAKI KWA WALIMU???????? Kazi kwenuuuuuuuuuuu.

3 comments:

Yasinta Ngonyani said...

karibu tena...ila ni vibaya kuondoka bila kuaga unajua...

Masangu Matondo Nzuzullima (MMN) said...

Karibu tena Mwanasaikolojia. Tunategemea kuona matunda ya kile ambacho umekipata katika masomo.

Huyo mchungaji Denis ni wa madhehebu gani?

Unknown said...

can we share a little bit in curriculum and psychology?