Saturday, December 27, 2008

Kwanini penzi unanitesa kiasi hicho.

Penzi ni kipofu. Penzi linatesa sana. Kwanini penzi linatesa? Mtaalam wa masuala ya mapenzi Pinig Huing wa china alibainisha kuwa penzi ni tamu kuzidi kila kitu hapa duniani na kuongeza kueleza kuwa penzi pia linaumiza sana.


Hii ni kweli kabisa ndugu yangu yakupasa kuanzia sasa hivi utambue kuwa penzi ni tamu ukijua hilo ninaimani utamdhamini mpenzi wako na utampenda zaidi. Ili kuhakikisha unamjali mpenzi wako yakupasa uonyeshe upendo kila unapokuwa na mpenzi wako.


Katika dunia ya wapendanao unatakiwa kumjali dear wa moyo wako ili ajui kuwa unamjali jambo ambalo litawafanya muishi kwa furaha na raha za dunia kuziona. Hupaswi kuona kwa mwenzako jinsi anavyomjali dear wake halafu na wewe uanze kumjali mpenzi wako.


Katika vitu vya kuzingatia katika kumuonyesha mpenzi wako unamjali ni kumbusu kila wakati, kumkumbatia kila wakati, kumhondomola ipasavyo huku ukitumia kila staili za kuhondomola, hapo utakuwa umemjali mamsapu wako ipasavyo na jambo hilo hatakusahau kamwe atakuwa anakukumbuka hata kama ukiwa kazini.

No comments: