Saturday, December 27, 2008

Zawadi ni chachu ya penzi


Nani alikuambia kuwa mtu ukimpa zawadi ya pipi utakuwa humpendi? nani alikuambia zawadi zenye thamani ndizo zinaonyesha ishara ya pendo?


Karlosia Hukou mwanasaikolojia wa nchini Korea aliwahi kuandika katika kitabu chake cha "Gift is Gift" mwaka 2006. Ambapo katika kutabu hicho alielezea kuhusu umuhimu wa zawadi kwa wapendanao.


Hukou alibainisha kuwa zawadi ni ishara ya upendo haijalishi zawadi ya thamani gani?, alieleza kuwa hata mpenzi wako ukimununulia nguo ya ndani kama anakupenda atazidi kukupenda zaidi.


Naye Sarah James wa Marekani aliwahi kubainisha katika tafiti (research) yake aliyoifa mwaka 2008 katika chuo cha Havard, alifafanua kuwa iwapo mpenzi wako utakuwa unamfanyia saplaisi ya kumnunulia zawadi ndogo ndogo kama pipi na kumpa huku ukimwambia "Mpenzi wangu pokea hii zawadi nimenunua kwa ajili yako dear" jambo kama hilo alisema linadumisha penzi.


Je, wewe unamununulia zawadi za aina gani mpenzi wago?

No comments: