WAKATI mwingine huwa unajisikia kumchoka mpenzi wako, kuchukua jukumu la kumuacha wako mpenzi, kumkaripia wako mpenzi, kumuona kama anakasoro fulani hivi, kumuona hakufai au hafai kuishi na wewe ikiwa pamoja na kutamani kuoa au kutafuta mwingine mpenzi.
Yote haya mambo huwa yanatokea kwa binadamu wa jinsia zote. Sasa nakuuliza kwanini unafikia hatua ya kufanya mambo kama hayo? Kama kweli uliamua kumpenda mpenzi wako ya nini tena kumchukia na kumuona hakufai?
Watalaam wa masuala ya mapenzi wanabainisha kuwa kumchukia mpenzi kunasababishwa na vitu vingi sana, ambapo mwanasaikolojia na mtaalam wa masuala ya love Haliet Julliu alifafanua katika kitabu chake cha "Bad Love - 2008" kuwa jambo la kwanza ambalo linamfanya mpenzi wako kukuchukia ni:
i)Uchufu wa mwili wako pia unapokuwa mchafu ndio unaongeza hatari ya kuchukiwa na mpenzi wako.
ii)Uchafu wa nyumba au chumba ambacho unakaa na mpenzi wako hasa hili linawahusu mwanawake, jambo hili huwa linawakera wanaume.
iii) Kupata mpenzi nje ya ndoa pia kunachakia mpenzi wako kukuchoka na kukuona hufai kisa kapata wa kumhodomola hasa akimpata anayejua mapenzi.
iv) Wewe mwenyewe kuwa mkali pindi unapomuona mpenzi wako nako kunachangia kumfanya atafute mwingine ambaye ni mpole ili apate kuliwazika zaidi kimahaba na,
v) Kuwa na wasiwasi wa kusalitiwa na mpenzi wako jambo ambalo huwa linazua mitafaruku kwa wapenzi na kusababisha kuchukizana na pengine kupelekea kuachana kabisa.
Kwahiyo nawashauri sana ndugu zangu mjitahidi kuepuka mambo kama haya ili kudumisha penzi zaidi.Sasa tujadiliane kuhusu suala hili na pia napenda kuuliza Je, penzi ni nini?
4 comments:
aaaaaaaaaaaaaah HAMU bwana. samahani nakusalimia tu mambo maana nina hamu siku nyingi sana hatusalimiana
Haya asante fresh mtu wangu lakini imetulia? unajua yasita amepotea kwenye blogu kwani siku hizi hatumi hata maoni
Ngoja nimtete kidogo. Yasinta yupo safarini rafiki yangu, kwahiyo alikuwa katika maandalizi ya kusafiri ndiyo maana unaona kapotea hivyo, lakini kaaga kwamba atakuwepo mara chache. Ngoja nitajaribu kumtisha kufungua kesi si unajua mimi ni wakili wa ndoto za usiku? ha ha ha ha Yasinta yupo nitakushtua mkuu
Ok fresh sana ninafurahi sana kukutana na waadishi wenzagu huria katika kibara hiki
Post a Comment