Sunday, March 21, 2010

Penzi ni Tamu Sana Jaribu Uone???



PENZI ni tamu sana kila mtu anatambua hilo, na kukoswa pendo ni uchungu sana katika maisha ya binadamu.

Pamoja na hayo yawezekana wewe unayesoma blogu hii na wewe unampango wa kumuacha mpenzi wako, kutokana na sababu mbalimbali lakini yote hayo ni sawa na kupotea ndugu yangu.

Nakuomba sana usimuache mke wako kwani daima ulishamutamkia kuwa unampenda na hutamuacha kamwe katika maisha yako! Kumbuka baada ya kumuacha mrembo bibie utapata nini au utafaidika na nini? Zaidi ya kuanza kujuta na kuumia roho yako?

Wapo wanaume wengi wanaoachana na wake zao matokeo yake wanaanza kujutia kitendo hicho.

Namkumbuka baba mmoja tajiri mkubwa katika jiji hili la Dar aliwahi kuja katika ofisi zetu za ushari ili kuomba ushari wa doa yake
Baada ya mke wake kuchoshwa na baba huyo na kuamua kurudi kwao Mwanza.

Sasa baada ya kuachwa baba huyo alianza kuumia zaidi na kuwa anashinda nyumbani badala ya kwenda kazini, jambo ambalo lilimpelekea kuja ofini kwetu kuomba ushauri wa kufanya ili mke wake arudi.
Nasi tulimpatia ushauri na tukamuita mke wake naye tukamupa ushauri wa umuhimu wa mke na mume katika ndoa, jambo ambalo liliwaunganisha na mpaka sasa wanaishi kwa amani na upendo wa ajabu.

Sasa ndugu yangu kumbuka kuwa mwanamke ni muhimu sana katika maisha yako, mwanaume ameumbwa kwa ajili ya mwanamke na mwanamke kwa ajili ya mwanaume sasa kunahaja gani ya kumtukana mke wako ambaye ni mzuri? Kunahaja gani ya kumfukuza mke wako anaye kupa penzi la dhati? Na kunahaja gani ya kuwa na msongo wa wawazo kisa mke wako mwenye penzi tamu kaondoka? Sasa mwambie mke wako nakupenda sana mke wangu na sitakuacha kamweeeee.

1 comment:

Anonymous said...

we chizi shauri vi2 vya maana