Sunday, November 23, 2008

Kusononeka sana


Ndugu msomaji na mfuatiliaji wa blogu yako ya saikolojia wataalamu wa saikolojia wanatuhabarisha kuwa binadamu anapokuwa na hudhuni sana anaweza kuwa na hatari ya kupata magonjwa mbalimbali ikiwemo kisukari, moyo, kutokwenda haja kubwa, kupunguza nguvu za mapenzi, kupungua uzito wa mwili, kuumwa kichwa sana, kupoteza mwelekeo katika mipango yako ya kiakili nk.


Kwahiyo ndugu unatakiwa kujitahidi kufurahia maisha yako kila wakati na unapojaribu kuufanya mwili wako kufurahi, lakini hautaki watalaamu wanakushauri kuwa fanya mazoezi au jichanganye na watu mbalimbali katika maongezi hudhulia ibada za dini na mikutano mbalimbali ya injili hapo utaona mabadiliko ndugu yangu.


Wataalamu wanakuambia hivi usisononeke sana hata kama umeachwa na mpenzi wako, au wewe ni masikini, huna uwezo darasani, sauti yako unapoongea ni mbaya, unapofanya kazi uliyoisomea unakosea, au unapokumbana na mikasambalimbali ya maisha just toa hiyo huzuni moyoni mwako na kuanza kufurahia maisha hata kama ni mabaya ukifanya hivi utazoea na utaona kama kawaida. "Mungu akubariki sana"

No comments: