Sunday, November 2, 2008

Uchungu wa Penzi

Penzi ni kitu ambacho kinauma sana, maumivu yake ni makali mno tofauti na maumivu mengine watu wengine wanapoachwa huwa wanadiliki hadi kulia! Hakika penzi huuma pale unapoachwa na mpenzi wako ambaye ulikuwa umemuweka katika roho yako.

Katika dunia hii watu wengi wameugua magonjwa mbalimbali kutokana na kuachwa. unapoachwa na mpenzi wako mara nyingi utakuwa umeathirika kisaikolojia kitendo ambacho kinaweza kukufanya kila wakati uwe unafikria mambo mengi sana. Ili kutibu ugojwa wa kujisikia mpweke la msingi ni kama wewe ni mwanafunzi tumia muda wako mwingi kujisomea kitendo ambacho kitakufanya umusahau mpenzi wako aliyekuacha. Kama wewe ni mfanyakazi labda katika ofisi tumia muda wako mwingi kujishughulisha na kazi za ofisini ukifnya hivyo hakika utasahau maumivu yataisha taratibu mengine ni kufanya mazoezi nk.

No comments: