"Najitahidi sana kumshauru mme wangu Leonard ili awe anawahi kurudi ili nimufaidi mme wangu lakini hataki kutekeleza ushauri wangu sasa ngoja kuna siku nitaenda kumchongea kwa bosi wake ili afukuzwe kazi nifaidi penzi lake kwa kuwa naye masaa yote" alisema dada mmoja ambaye anafahamika kwa jina la Mariam Sabaganga mkazi wa Mwanza.
Pengine wa wewe unamawazo kama hayo kutokana na mme wako kutingwa na kazi nyingi na hatimaye kushindwa kuwa anawahi kurudi nyumbani mapema. Nakuomba usiwe na wivu kiasi hicho kwani kazi ya mme wako ndiyo inawafanya kuishi au kujiongezea kipato nyumbani kwenu.
"Ninajuta sana kutokana na watoto wetu kushindwa kusoma kutokana na mme wangu kufukuzwa kazi baada ya kumchongea kwa bosi wake kuwa anatabia ya kumuibia bosi pesa za kampuni yake na kuleta nyumbani na zingine kuweka benki" alisema mama Aisha mkazi wa Area "D" mjini Dodoma baada ya kujuta kutokana na kumsababishia mme wake kufukuzwa kazi kwa wivu wa mapenzi.
Aliendelea kusema kuwa "Kama ningejua kama tutateseka kiasi hiki, yaani tunalala njaa huku watoto hawaendi shule, kwakweli inaniuma sana na ninamuomba Mungu atusaidie angalau tupate pesa za kuwasomesha Aisha, Ben na Hamis!"alisikitika mama huyo.
Sasa je, na wewe unawivu wa kiasi hicho? Toa maoni yako ili kusaidia kufanikisha kwa utafiti ambao unafanya na shirika la Tanzania Women Reseach.